Friday , 15th Jun , 2018

Mamlaka nchini Kenya, imekamata mitumbwi mitatu na zana nyingine za uvuvi zinazomilikiwa na watanzania ambazo zilikuwa zinafanya uvuvi haramu katika Bahari ya Hindi upande wa nchi ya Kenya.

Kwa mujibu wa Citizen Kenya imeripoti leo Juni 15, 2018 na kuongeza kuwa mwenyekiti wa pwani ya Kibro bwana Samwel Magese amesema kuwa wavuvi hao hawakuwa na kibali chochote cha uvuvi ingawa walifanikiwa kutoroka.

“Ukamataji huu muendelezo wa adhabu kwa wavuvi haramu katika pwani ili kuleta usalama katika sekta ya uvuvi” amesema Magese.

Bwana Magese ameongeza kuwa operesheni katika eneo hilo itaendelea ili kudhibiti uvuvi haramu na kuongeza kuwa wavuvi wote wanatakiwa kuwa na kitambulisho cha utaifa pamoja na barua rasmi ya eneo wanalotoka.

Disemba 2017 jumla ya wavuvi 27 kutoka nchini Tanzania walikamatwa katika pwani hiyo ikiwa ni agizo la Rais Uhuru Kenyatta baada kusimamisha leseni zote za uvuvi  kutoka nje ya nchi hiyo mpaka zitakapotimiza vigezo vya nchi hiyo.