Wednesday , 22nd Jun , 2016

Tanzania imetakiwa kushugulikia upungufu wa lishe katika bidhaa za vyakula ili kuboresha afya za watu wake hususan watoto kwani maendeleo endelevu huendana lishe bora.

Washidni wa tuzo ya Nestle kushoto ni zao la Vanila kutoka Tanzania na zao la Muhogo kutoka Cameroon

Ushauri huo umetolewa na Meneja Udhibiti na Sayansi wa Vyakula na Vinywaji wa kampuni ya bidhaa za vyakula ya Nestle Tanzania, Bi. Marsha Makatta Yambi wakati wa utoaji wa tuzo kwa kampuni inayofanya kazi karibu na jamii na kuleta ongezeko la thamani katika mazao ijulikanayo kama Creating Shared Value inayoshindaniwa duniani kote.

Katika tuzo za mwaka huu kampuni ya kitanzania ya Natural Extracts Industries ,NEI ,kutoka mkoani Kilimanjaro imefanikiwa kuwa mshindi wa pili duniani na kujinyakulia kiasi cha Dola laki mbili miongoni mwa makampuni 450 yaliyoshiriki shindano hilo.

Bi Marsha Yambi amesema hii ni hatua kubwa kwa Tanzania kwani fedha hizo zitatumika zaidi kuwaendeleza wakulima wa zao la Vanila wilayani Moshi na kuzitaka taasisi na kampuni mbalimbali zilizopo katika sekta ya kilimo kushiriki mashindano hayo kwa ajili ya kujipatia fedha za kukuza miradi yao na baada ye kuisaidia jamii.