anafaa kuwaongoza kwa nafasi hiyo.
Kadhalika Kikwete, amesema yeye siyo mgombea wa nafasi hiyo, japokuwa amekuwa akisikia watu wanasema na amesoma kwenye mitandao watu wakijadili kwamba ni miongoni mwa wanaopewa nafasi kubwa ya kushinda nafasi hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari waliomuomba kuzungumzia taarifa hizo ambazo zimekuwa zikisambaa katika mitandao ya kijamii, baada ya kufungua mkutano wa Kikanda wa kujadili mabadiliko ya tabia nchi jijini Dar es Salaam, Kikwete amesema yeye ametumika vya kutosha katika nafasi kubwa, hivyo hana mpango kwa kukaa chini na kuandika barua ya kuomba kazi tena.
“Na mimi nimekuwa nikisikia taarifa hizo, wengine wanasema nimepewa nafasi ya tatu, wengine wanasema ninapewa nafasi kubwa kushinda nafasi ya Katibu Mkuu, lakini mimi hata siyo ‘Candidate’ wa nafasi hiyo, wal sijaomba” alisema Kikwete.
“Ila kama wataafrika watakaa chini wakaona wanahitaji msaada wangu wakaniteua au wakaona wanahitaji ushauri wangu niko tayari kuwatumikia na ninaahidi kwamba siwezi kukataa kuwatumikia wa Afrika” amesema Mhe Kikwete






.jpeg?itok=uqe_Ivr6)