Jeshi la Polisi Nchini Tanzania limewaonya madereva wote wa vyombo vya moto nchini kuzingatia sheria za barabarani hasa katika kipindi hiki cha Sikukuu za mwisho wa mwaka ili kuepusha ajali na kuwataka wazazi kuwalinda watoto wao katika kipindi hiki cha Sikukuu.
Onyo hilo limetolewa leo Jijini Dar es salaam na msemaji wa Jeshi hilo Advera Bulimba na kuongeza kuwa jeshi hilo pia litawakamata madereva wa bodaboda wote wanaokatisha wakati taa nyekundi zinawaka pamoja na wale wanaopakia watu wengi maarufu kama mshikaki pamoja na abiria waliowapakia pia watakamatwa.
Aidha, Bulimba amewataka wananchi kutoa taarifa za viashiria vya uvunjifu wa sheria wakati huu wa msimu wa Sikukuu ikiwa na pamoja na kutoa taarifa za watu wote wanawashuku kuwa ni waalifu. Pia Jeshi la Polisi limewakumbusha wamiliki wa kumbi za starehe, magari ya abiria kutojaza watu kupita uwezo unaotakiwa kisheria.