Tuesday , 2nd Feb , 2016

Kila Halmashauri nchini yatakiwa kutenga asilimia tano ya mapato yake ya ndani kwa kila mwaka wa fedha kwa ajili ya vijana na kutekeleza shughuli mbalimbali za kuwawezesha vijana kujiajili wenyewe.

Naibu waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI, Seleman Jaffo

Hayo yamesemwa na naibu waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI, Seleman Jaffo wakati akijibu swali la mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki Mhe. Mgumba Tebweta aliyetaka kujua lini serikali itaanzisha kituo maalum cha kuwawezesha vijana kujiajiri.

Naibu waziri ameongeza kuwa mpango huo ni endelevu, na tayari serikali imepitisha mpango wa kuwawezesha vijana kwa kuwatengea fedha shilingi bilion 233 kwa mwaka wa fedha 2015/2016 kwa ajili ya kuwasaidia vijana takriban 71,408 kupata ajira za kudumu.

Aidha amewataka wabunge kusimamia na kutekeleza maamuzi wanayokubaliana kwenye vikao vyao vya halmashauri zao.