Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego.
Akizungumza katika kikao kazi na watumishi wa halmashauri ya Mtwara, Mikindani ambapo alisomewa bei ya sukari katika halmashauri hiyo kuwa imepanda hadi kufikia sh 2,500 mpaka 3,500 kwa kilo moja ya Sukari.
Mhe. Dendego amesema kuwa suala la kusimamia tatizo hilo iwe ya watumishi wote na wala sio kuiachia ofisi ya mkuu wa mkoa au mkuu wa wilaya pekee, hivyo waweze kuwasimamia wasambazaji wakuu wa Sukari kuona kama wanaifikisha sokoni kama inavyohitajika.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amegiza kufanya uhakiki wa wafanyabiashara, wanaouza bidhaa mbalimbali ndani ya masoko ya halmshauri ya manispaa ya Mtwara Mikindani ili kukusanya ushuru kwa kiwango kinachotakiwa.
Bi. Halima Dendego amesema kuwa mapato mengi yanapotea kutokana na mfumo wa ukusanyaji ushuru kubagua ambapo kuna watu wengine hawalipi kodi vile inavyotakiwa hivyo kuikosesha serikali mapato.