Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya udhibiti wa nishati,maji nchini Felix Ngalamgosi.
Akizingumza na waandishi wa Habari jana Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngalamgosi, amesema Mtwara,Songea na Ruvuma ambapo kumekuwa na uhaba wa mafuta ya taa,Magari yameshapeleka mafuta.
Aidha Mkurugenzi huyo amesema kuwa serikali imeshakusanya maoni ya wadau ili kutoa fursa kwa kampuni za Tanzania kushiriki kupata zabuni kwa ajili ya kuleta mafuta nchini.
Ngalamgosi amewatoa hofu wananchi kwamba nchi haitaingia katika uhaba wa mafuta ya taa kwa kuwa kuna mafuta ya kutosha yanayokidhi mahitaji mbalimbali kwa muda wa siku 16.
Akizungumza chanzo cha uhaba wa mafuta ya taa Ngalamgosi amesema chanzo cha upungufu huo ni kutokana na meli iliyobeba mafuta ya Petroli na ya ndege kuachanganyika hivyo kusababisha kuchafuka kwa matangi na mabomba yote.