Tuesday , 19th Apr , 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo amezindua daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam, ambapo amesema kukamilika kwa daraja hilo ni hatua kubwa ya katika maendeleo ya Jiji na nchi kwa ujumla.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipotembelea daraja hilo wakati ujenzi

Akizungumza katika uzinduzi wa daraja hilo rais Dkt. Magufuli amesema kuwa daraja hilo licha ya kuunganisha wananchi wa Kigamboni lakini pia litaunganisha watu wote ikiwa ni pamoja na kuleta maendeleo ya nchini.

Dkt. Magufuli amesema kuwa daraja hilo limekuwa kama mkombozi wa wananchi wa Kigamboni amependekeza ipewe jina la baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ili kumuenzi kiongozi huyo.

Dkt. Magufuli amewataka wananchi kulitumia daraja hilo kwa ajili ya maendeleo na kuwataka watumiaji wa vifaa vya usafiri ikiwemo, Baiskeli, Pikipiki, Bajaji na Magari lazima walipie ili kumaliza deni ambalo serikali imekopa kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo.

Aidha, Dkt. Magufuli amesema wananchi hawana budi kusifu ujenzi wa daraja hilo na huku akiwataka waandishi wa habari watumie kalamu zao kulitangaza daraja hilo na rasimali nyingine za nchi ambazo ni vivutio vya utalii.

Vilevile Dkt. Magufuli amesema daraja hilo litakuwa na wafanyakazi karibu 300 ambao watakuwa wanafanya shughuli mbalimbali ikiwemo usafi pamoja na ulinzi wa daraja hilo.

Daraja la Kigamboni lilianza kutumika tarehe 16 Aprili, 2016 lina urefu wa mita 680 na barabara unganishi (approach roads) upande wa Kurasini na Kigamboni zenye urefu wa Kilometa 2.5. ambapo Ujenzi wa daraja hilo umefanywa na Kampuni ya China Railway 15 Group ilishirikiana na Kampuni ya China Bridge Engineering Group ambapo limegharimi zaidi ya shilingi bilioni 250 za Taanzania.