Friday , 1st Apr , 2016

Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally, amekabidhi madawati 200 kwa shule 9 za sekondari katika halmashauri ya Mji wa Nanyamba, ambayo yamenunuliwa kwa kutumia mapato yake ya ndani.

Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally

Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally, amekabidhi madawati 200 kwa shule 9 za sekondari katika halmashauri ya Mji wa Nanyamba, ambayo yamenunuliwa kwa kutumia mapato yake ya ndani.

Akizungumza wakati wa kukabidhi madawati hayo, Mkuu wa Wilaya huyo amewataka waku wa shule hizo kuhakikisha madawati hayo yanatunzwa vizuri ili yaweze kudumu kwa muda mrefu na kutumiwa na wanafunzi wengine hapo baadaye.

Aidha, amesema halmashauri hiyo ilikuwa inakabiliwa na upungufu wa madawati 1,387 lakini baada ya kuanza jitihada za kuhamasisha utatuzi wa uhaba wa vifaa hivyo sasa tatizo limepungua mpaka kufikia idadi ya madawati 840.

Kwa upande wake, Afisa Elimu ya Sekondari katika halmashauri hiyo, Bumi Kasege, amesema hali ya upatikanaji wa viti na meza kwa shule za sekondari sio nzuri, na kwamba hali hiyo inasababishwa na ongezeko la wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2016.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya Fatma Ally akikabidhi madawati
Afisa elimu sekondari katika halmashauri ya Nanyamba Bumi Kasege, akizungumzia hali ya Madawati