Tuesday , 1st Jul , 2014

Uongozi wa jiji la Dar es Salam umesema uko mbioni kujenga hospitali ya wazazi itakayoweza kuwahudumia wakazi wa wilaya za Kinondoni, Ilala na Temeke kwa pamoja ili kuepukana vifo vinavyotokana na upungufu wa vituo vya kutolea huduma za uzazi.

Kaimu mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Ilala Raymond Mushi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi amesema maandalizi ya ujenzi huo yameanza huku utaratibu wa kutambua eneo la ujenzi na wafadhili ukiendelea.

Wakati huio huo Bw. Mushi amewaasa wahudumu wa afya kuacha kutoa huduma za ubaguzi kwa wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na kuwataka wanachama kutoa taarifa ili waweze kuchukuliwa hatua stahiki.

Ujenzi wa hospitali hiyo ni mafanikio makubwa ya kampeni za mda mrefu zinazoendeshwa na asasi mbali mbali za kiraia za kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano, moja kati ya malengo ya milenia ambalo Tanzania imeonekana kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.