Friday , 12th Sep , 2014

Mwenyekiti wa kituo cha Demokrasia Tanzania TCD, Mh. John Cheyo ametaka makubaliano waliyofikia kati ya kituo hicho na rais kuhusuiana na Mchakato wa Katiba yaheshimiwe kwa kuwa ndio maamuzi ya mwisho ya yama vyote vinavyoshiriki uundwaji wa katiba.

Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania TCD John Cheyo (kushoto) akiteta jambo na James Mbatia ambaye ni mmoja wa viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi - UKAWA.

Cheyo amesema kati ya maamuzi waliyokubaliana kati ya Rais kati na Kituo hicho ambacho pia kinajumuisha na Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA ni bunge la Katiba la sasa linaloendelea liweze kuendelea mpaka litakapopata katiba itakayopendekezwa na kisha mchakato huo usitishwe mpaka baada ya uchaguzi mkuu Mwakani.

Aidha Mh. Cheyo amesema kuwa walikubaliana kuendelea kwa bunge hilo kwa linaendeshwa kwa mujibu wa sheria hivyo Rais asingeweza kulisitisha ghafla na hivyo kuwataka viongozi wenzake wa upinzani kuheshimu maamuzi hayo.

Kauli ya Cheyo imekuja siku moja baada ya viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA kutaka bunge hilo lisitishwe kuepuka kile walichokiita kuwa matumizi holela ya fedha za umma ambazo wamesema kimsingi ziungeweza kutumika kuboresha huduma za kijamii.