Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

CHADEMA yafunguka kuhusu kujitoa uchaguzi wa kesho

Friday , 16th Feb , 2018

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni kuwa imejitoa katika uchaguzi mdogo wa marudio kwenye jimbo la Kinondoni, Siha na kata nane nchini na kuwataka wananchi kuzipuuza taarifa hizo wazipatapo.

Akizungumza na mwandishi wa EATV,  Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje- CHADEMA John Mrema amesema kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote na kudai wanaofanya hivyo ni kundi cha watu wachache wenye lengo la kutaka kupotosha umma ili kesho wasiende kupiga kura.

"Taarifa hizo ni za uongo zinasambazwa na watu ambao wameshashindwa naomba watu wazipuuze. Tunapozungumza sasa hivi Mwenyekiti wa chama Mhe. Mbowe anahitimisha kampeni katika jimbo la Kinondoni na Mhe. Lowassa yupo kule Siha nae anahitimisha kampeni",amesema Mrema.

Pamoja na hayo, Mrema ameendelea kwa kusema "tunaomba kuwaambia wananchi na wanachama wa CHADEMA kuwa hiyo sio barua yetu na pia sio utaratibu kwa mujibu wa kanuni mwenyekiti wa chama kuandika barua ya kujitoa kama mtu mwenye haki ya kujitoa ni mgombea. Kwa hiyo hata hao watu walioandika hiyo barua hawajui sheria za uchaguzi zinasemaje".

Kwa upande mwingine, Mrema amezidi kuwasisitizia wananchi kuzipuuza taarifa zozote zinazotoka sasa kuhusu kutoshiriki uchaguzi huku akiwaomba wananchi katika Jimbo la Kinondoni na Siha kujitokeza kwa wingi kesho kushiriki kupiga kura kwa sababu ni haki yao ya msingi.

HABARI ZAIDI

Bujukano Mahungu John, Mwenyekiti wa Umoja wa Waganga na Wakunga wa Tiba Asili Tanzania

Waganga wa jadi waungana kukemea ukatili, Geita

Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania

Mvua zilizoambatana na upepo zimeua watu watano TZ

Muonekano wa Eneo la Somanga baada ya Mawasiliano kati ya Lindi na Dar es Salaam kurejeshwa.

Mawasiliano yarejeshwa barabara ya Dar - Lindi

Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga

Kituo cha kupoza umeme kujengwa Tunduma

Mkuu wa Usalama Barabarani mkoa wa Songwe Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Charles Bukombe, akizungumza na abiria

"Fungeni mikanda muda wapo safarini" - SSP