Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

CHADEMA watangaza jeuri

Wednesday , 6th Dec , 2017

Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Kinondoni, Waziri Muhunzi amesema hawana hofu juu ya aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Maulid Mtulia (CUF) kuhamia CCM kwani wako imara na wanasubiri taratibu za kutangazwa siku ya uchaguzi ili waweze kutetea kiti hicho.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatano na alipokuwa akituma salamu kwa wananchi wa jimbo la  kuwataka kuwa wavumilivu baada ya aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Maulid Mtulia kujiuzulu uongozi mwishoni mwa wiki iliyopita.

"Wananchi wa Jimbo la Kinondoni wako salama kwani Mtulia hakuondoka na wanachama hivyo tuko vizuri na hatujasambaratika kama ilivyodaiwa hapo awali. Ikitokea wanachama wanaandamana na wao kurudi CCM basi tutajua tatiazo liko wapi. Hapa tulipo tunasubiri tu Tume ya Uchaguzi itangaze ni lini uchaguzi ili tuingie kazini," amesema Muhunzi.

Ameongeza "Lazima tulitetee jimbo hili na uzuri aliyekuwa Kampeni Meneja wa Mtulia 2015 ni mimi hapa na sijahama kwa hiyo lazima tuhakikishe jimbo linabaki kwenye mikono ya upinzani. Mbunge wa jimbo hili bado ataendelea kutoka UKAWA licha ya usaliti aliyoufanya Mtulia ili hali CHADEMA ilipigania kila hatua kuhakikisha amepata nafasi hiyo katika uchaguzi wa 2015.

"CCM hawako salama wasifikiri kumchukua Mtulia wamemaliza Wilaya ya Kinondoni, wanachama wapo na wataendelea kuwepo ndani ya CHADEMA," amesema.

 

HABARI ZAIDI

DCP David Misime, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania

Mtoto atekwa na mzazi wake ili ajipatie milioni 20

Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Anton Sabasaba Akizungumza wakati alipohudhuria kikao cha wazazi katika Shule ya Msingi Elisabane Mei 24, 2024

Wototo wafuatiliwe na kulindwa kama mboni - Anton

Maduka ya Wafanyabiashara yakiwa yamefungwa

Wamiliki wa maduka Mebya wafunga biashara zao

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Agustino Senga

Polisi waambiwa kazi yao ni kazi ya Mungu

Kiwanda cha sukari Mtibwa

11 wafariki dunia kiwanda cha Mtibwa

Wilman Kapenjama Ndile, Mkuu wa Wilaya ya Songea

DC Kapenjama ataka uaminifu kwa wakulima Songea

Bashiri Mohamed (35) Mwenye Koti Jeusi akiwa anafikishwa Mahakamani Ilemela, Jijini Mwanza

Aliyezini na binti yake apandishwa kizimbani