Thursday , 23rd Jun , 2016

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kwamba serikali itaanza kupeleka fedha za miradi ya maendeleo katika halmashauri ili ahadi zilizoahidiwa zianze kutekelezwa kwa vitendo.

Majaliwa ameyasema hayo alipokuwa akijibu swali la Mbunge Hamida Mohamed Abdala aliyetaka kujua mkakati wa serikali katika kuhakikisha kwamba serikali inapeleka fedha kwa wakati na kuhakikisha usimamizi wa fedha hizo.

Akijibu swali hilo Waziri Mkuu Majaliwa amesema serikali ina nia ya dhati ya kuhakikisha fedha zilizotengwa kwa ajili ya maendeleo zinatoka kwa wakati na kusimamiwa ifuatavyo.

''Watendaji watumie fedha za maendeleo katika miradi iliyokusudiwa na kuhakikisha miradi ina thamani ya fedha zilizotengwa kwani serikali haitasita kumchukulia hatua mtumishi yeyote ambaye hatatimiza wajibu wake katika kusimamia miradi iliyochini yake''-Waziri Mkuu Majaliwa.