Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Phillip Mpango
Muswada huo unalenga kutunga sheria ya fedha kwa ajili ya kuweka, kurekebisha, kupunguza pamoja na kufuta kodi, ushuru ada na tozo mbalimbali kwa lengo la kuboresha ukusanyaji wa kodi.
Akiwasilisha Muswada huo leo Bungeni mjini Dodoma, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Phillip Mpango amesema katika marekebisho hayo, ni pamoja na kupunguza misamaha ya kodi isiyo na tija, kupunguza kiwango cha chini cha kutoza kodi ya mapato yatokanayo na ajira, kuiwezesha Mamlaka ya Mapato Tanzania kukusanya kodi ya majengo badala ya halmashauri na kuweka sharti kwa kampuni za simu kujiorodhesha katika Soko la Hisa ili watanzania wanunue hisa.
Wakizungumza na EATV baadhi ya wabunge wamekuwa na maoni mbalimbali kuhusiana na muswada huo kama ifuatavyo