
Baadhi ya mashtaka aliyosomewa Gugai anayedaiwa kumiliki viwanja 37, maghorofa saba, nyumba za kawaida tisa, magari matano pamoja na pikipiki, ni pamoja na kutakatisha fedha, kughushi fedha pamoja na kudanganya kuhusu mali anazomiliki.
Gugai alijisalimisha mwenyewe hapo jana baada ya TAKUKURU kutangaza dau la milioni 10 kwa yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwake, kwani walikuwa wakimtafuta bila mafanikio.