
Jokate Mwegelo
Taarifa hiyo imetolewa na Kaimu mkurugenzi wa uchunguzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), nchini Ali Mfulu, ambapo amesema kuwa Chuma alikamatwa na maofisa wa TAKUKURU, baada ya kupokea taarifa kutoka Kisarawe.
Mfuru ameongeza kuwa, walifanikiwa kumkamata ikiwa ni wiki takribani tatu, zikiwa zimepita tangu wautangazie umma kuhusu, kukamatwa kwa matapali wengine sita walioshirikiana kufanya utapeli.
''Kati ya watuhumiwa hao, wanne walijifanya ni maofisa wa Takukuru wa vyombo vingine vya dola na wawili walitoka katika kampuni ya simu''
Na kwamba uchunguzi huo, umebaini kuwepo kwa mtandao mkubwa, unaohusisha wafanyakazi wa ofisi mbalimbali zikiwemo za Serikali.