Wednesday , 9th Mar , 2016

Watu watu wamefariki dunia na wengine 19 kujeruhiwa vibaya katika ajali ya gari iliyohusisha magari matatu likiwemo basi dogo la abiria maarufu kama daladala iliyotokea leo jijini Dar es Salaam.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Lucas Mkondya amesema kuwa ajali hiyo imetokea leo asubuhi eneo la Tabata Sukita ambapo amesema chanzo cha ajali hiyo ni lori la mchanga kuligonga daladala kwa nyuma na kuhamia upande wa pili wa barabara na kugongana uso kwa uso na Lori lililokuwa limebeba Ng'ombe.

Kamanda Mkondya amesema madhara ya ajali hiyo ni makubwa sana baada ya kupelekaa vifo vya watu watatu papo hapo na wengine 19 kujeruhiwa na kuongeza kuwa majeruhi wote wamewahishwa katika hospitali ya amani kwa ajili ya matibabu zaidi.

Aidha Kamanda Mkondya ameongeza kuwa bado jeshi la polisi linaendelea kupepeleza tukio hilo na kujua chanzo cha delreva wa lori la mchanga kugonga daladala ambapo amesema baada ya uchunguzi kukamilika jeshi hilo litatoa taarifa kamili juu ya tukio hilo.