Moja ya Wahanga katika tukio la shambuli Mjini Bangladesh.
Vikosi vya Bangladesh vimekomesha mzingiro wa saa 10 wa makahawa huo ambapo raia 35 walishikiliwa mateka na wapiganaji waliokuwa na silaha wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa Dola la Kiislam(IS).
Kiongozi wa operesheni za kijeshi Brigedia Jenerali Nayeem Ashfaq Chowdhury amesema kuwa Kati ya magaidi saba, sita wameuawa na tumemkamata mtuhumiwa mmoja.
Jeshi la Bangladesh limesema raia hao wa kigeni 20 ambapo ni mchanganyiko wa Wajapani na Waitaliana wameuwawa kikatili wengi kwa kuchomwa visu na kukatwa katwa.


