Wanachama zaidi ya 500 wa CHADEMA wahamia ACT
Zaidi ya wanachama 500 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakiwemo viongozi wa kata mbalimbali katika wilaya ya Ludewa mkoani Njombe, wamekihama chama hicho na kujiunga na chama cha ACT-Wazalendo.
