K.O wa bondeni kutembelea Dar na Nai
Rapa mkali kutoka Afrika Kusini, K.O. anajipanga kwa ajili ya ziara yake kubwa Afrika Mashariki, ambapo ataitembelea Tanzania wiki ijayo kuanzia tarehe 14 mpaka 16 kabla ya kufanya ziara kama hiyo nchini Kenya tarehe 17 mpaka 20 mwezi huo.

