Ligi kuu bara kuwakutanisha Simba na Mtibwa kesho
Baada ya kusimama kwa wiki mbili kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar, Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara mzunguko wa kumi na nne (14) unatarajiwa kuendelea hapo kesho wikiendi hii kwa michezo 8 kuchezwa katika viwanja mbalimbali.