JPM aanza kuhudhuria Mkutano wa 28 wa AU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 29 Januari, 2017 ameanza kuhudhuria mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) unaoendelea Mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.