"Maalim Seif alizuia fedha za CUF"- Sakaya
Kaimu katibu mkuu wa CUF upande wa Profesa Lipumba, Magdalena Sakaya amemshukia Maalim Seif na kudai alikuwa na lengo la kukiua chama hicho, ndio maana aliweza kuzuia chama kisipate ruzuku kwa nchi nzima baada ya mgogoro wa mwaka 2016.