Makonda asitisha zoezi la Usafi Jumamosi
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda leo ametangaza rasmi kuondolewa kwa kipengele kilichokuwa kikiwataka wafanyabiashara kufunga maduka siku Jumamosi hadi Saa nne asubuhi kwaajili ya usafi na badala yake jukumu amelikabidhi kwa zaidi ya Vijana 4,000 wa JKT.