Sababu za ACT kutokukubalika na wanawake
Katibu wa Itikadi na Uenezi Chama cha ACT - Wazalendo, Ndg. Ado Shaibu amedai sababu kubwa ya chama chao kuonekana hakikubaliki na wanawake wengi ni kutokana na mazingira yasiyo rafiki ya kufanya siasa za upinzani yalivyo nchini na kwamba hayavutii wanawake.