'Ambulance' yenye mirungi, Ummy Mwalimu aamua
Ikiwa zimepita siku mbili tangu kuripotiwa kwa tukio la kukamatwa kwa gari la kubebea wagonjwa ‘Ambulance’ likiwa limebeba shehena ya mirungi, Wilayani Tarime mkoani Mara, Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameagiza kusimamishwa kazi wote waliohusika.