IGP Sirro awataka viongozi wa dini kufanya doria
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amewaomba Viongozi wa dini nchini kuendelea kufanya doria za kiroho huku Jeshi hilo likiendeleza doria za kimwili kwa pamoja ili kuukabili uhalifu ikiwemo mauaji yanayosababishwa na wivu wa mapenzi yaliyoshamiri siku za hivi karibuni.