Kocha wa Mashujaa FC aweka wazi kilichoiua Simba
Kocha wa timu ya soka ya Mashujaa ya mkoani Kigoma Tuga Manyundu, amesema nidhamu ya mchezo ndio sababu ya kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Mabingwa wa Tanzania Bara Simba SC katika mchezo wa raundi ya tatu michuano ya Azam Sports Federation Cup.

