Wanne Sprite Bball Kings wateuliwa timu ya taifa
Shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania (TBF) kupitia kwa Rais wake, Phares Magesa limesema kuwa Januari 14 hadi 18, 2020 timu ya taifa ya kikapu itashiriki mashindano ya kufuzu kucheza kombe la Afrika kwa wanaume, yatayofanyika Nairobi, Kenya.
