CCM yasema haitakosea tena jimboni kwa Msigwa
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt Bashiru Ally, akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Iringa, amewahakikishia wanachama wa CCM kuwa chama hicho hakipo tayari kupoteza jimbo la Iringa Mjini, kama ilivyofanyika miaka michache iliyopita.