Kauli ya CHADEMA kuhusu mgombea Urais
Chama cha CHADEMA kupitia kwa Mkuu wa Idara ya Mawasiliano wa chama hicho, Tumaini Makene, kimesema kuwa mpaka sasa hivi hakuna tangazo lililotoka ambalo, linawapa nafasi watangaza nia za kugombea Urais ndani ya chama hicho, kuwasilisha taarifa zao kwa Katibu Mkuu wa chama hicho.