Watendaji wa Vijiji wadaiwa kupiga Mamilioni
Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Daudi Sichone ametangaza kuwafukuza kazi pamoja na kuwapeleka mahakamani watendaji wa vijiji wanaokusanya mapato na kutowasilisha mapato hayo benki kwa ajili ya utekelezaji wa matumizi mbalimbali ya halmashauri hiyo.