"Mbowe arudishe Milioni 2 na wenzake wote" - Spika
Spika Job Ndugai, amemtaka Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, kurudisha kiasi cha zaidi ya Shilingi Milioni 2, alizolipwa na Bunge kabla ya kuanza utoro na wabunge wenzake na kwamba wasipofanya hivyo hawataruhusiwa kuingia bungeni, huku pia akiwataka kurudi Bungeni haraka sana