Baba adaiwa kumuua mwanaye kisa Shilingi mia tano
Mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Anthony Lyala mkazi wa kijiji cha kisesa A kata ya Bujora wilayani Magu mkoani Mwanza anatuhumiwa kumpiga hadi kumsababishia kifo mwanae Agness Anthony mwenye umri wa miaka minane kwa madai ya kupoteza shilingi mia tano.