Jumatatu , 1st Jun , 2015

Zoezi la uandikishaji kwenye daftari la wapigakura kwakutumia mfumo wa -BVR- linaendeleo vizuri katika baadhi ya mikoa hapa nchini.

Akithibitisha kuendelea vizuri kwa zoezi hilo Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji mstaafu 'DAMIAN LUBUVA' leo ametembelea katika vituo mbalimbali mkoani Dodoma baada ya kutembelea mkoa wa SINGIDA na kusema zoezi hilo litamalizika katika muda uliopangwa.

Amesema mikoa ya Geita, Mwanza, Shinyanga na Simiyu itaanza kuandikisha Juni, 2 hadi Julai, 4 wakati mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Mara na Manyara itaanza Juni 12 hadi Julai, 12.

Amekemea baadhi ya vijana ambao wamegeuza zoezi hilo kama njia mojawapo ya kujipatia kipato ambapo wanawahi katika vituo na kupanga foleni kama kawaida na kisha baadae kuuza nafasi zao kwa watu wenye haraka ya kujiandikisha.