Mahakama ya Nigeria imemhukumu Nnamdi Kanu, kiongozi wa harakati za kujitenga za Indigenous People of Biafra (IPOB), yaani Watu wa Asili wa Biafra, kifungo cha maisha jela baada kwa mashtaka saba yanayohusiana na ugaidi.
Hukumu hiyo iliyotolewa jana Alhamis inafuatia kesi iliyodumu takriban muongo mmoja, ambayo imechochea kujitenga kwa kusini-mashariki mwa Nigeria.
Jaji James Omotosho amesema kuwa Kanu alihamasisha mashambulizi dhidi ya vikosi vya usalama na raia kupitia matangazo na maagizo yake kwa IPOB.
Jaji huyo alikataa ombi la mawakili wa serikali la kumpa Kanu hukumu ya kifo, akisema hukumu ya kifo duniani kote inakosolewa na jamii ya kimataifa, hivyo kutokana na hilo na kwa maslahi ya haki, na kumhukumu kifungo cha maisha akiongeza kuwa licha ya kiburi na kutokuwa na majuto kwa Kanu, kulikuwa na ulazima wa kuchanganya haki na huruma.
Mbali na hukumu ya kifungo cha maisha, Kanu pia amepata kifungo cha jumla cha miaka 25 kwa mashtaka mawili, bila uwezekano wa faini, yote yakiendana na hukumu ya kifungo cha maisha. Ana muda wa siku 90 kukata rufaa.
Kanu, ambaye amekuwa gerezani tangu kukamatwa tena Kenya mnamo 2021, aliwalaumu mawakili wa serikali kwamba kupelekwa kwake kinyume cha sheria kulipunguza uwezekano wa kupata hukumu ya haki.
Hukumu hii inatokea baada ya mchakato wa kisheria wa miongo kadhaa, ulihusisha majaji wanne tofauti.

