Jumatano , 29th Apr , 2015

Baadhi ya wanafunzi mkoani Njombe hawajui kuimba wimbo wa taifa na hivyo kuboronga walipo imba wimbo huo mbele ya mkuu wa mkoa wakati wa uzindizi wa tuzo ya elimu ya mkuu wa mkoa.

Baadhi ya wanafunzi waliohudhuria katika Tuzo ya Elimu ya Mkuu wa Mkoa Mkoani Njombe.

Wakiimba wimbo huo kwa kupishana beti katika uzinduzi wa tuzo hiyo wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wangine wakisema Mungu ibariki Afrika wenzao wanasema Mungu Ibariki Tanzania.

Mkanganyiko huo umetokea wakati wa ufunguzi wa hafla ya uzinduzi wa tuzo ya taaluma ya mkuu wa mkoa ambayo ni kwa mara ya kwanza kutolea mkoani humo na Nyanda za juu Kusini.

Akisoma taarifa ya elimu ya mkoa wa Njombe Afisa elimu mkoa wa Njombe Said Nyasiro amesema kuwa wanafunzi zaidi ya asilimia 20 ya wanafunzi wanaonza darasa la kwanza hushindwa kufifika darasa la saba na kuwa wanao anza kidato cha kwanza kati yao asilimia 40 hawafiki kidato cha nne.

Akizungumzia tuzo hiyo mkuu wa mkoa wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi amesema kuwa tuzo hiyo inalengo la kuongeza ufauru kwa wanafunzi wa mkoa huo na kuuweka hamasa kwa walimu kuongeza juhudi.

Dkt. Nchimbi amesema kuwa tuzo hiyo inalenga kufanya mkoa wa Njombe kushika nafasi ya kwanza kitaifa wakati kwa mwaka wa jana mkoa huo ulishika nafasi ya tano kitaifa.

Kwa upande wa mmoja wa walimu ambao shule zao zimepata zawadi ya Pikipiki na kutakiwa kusajili kwa jina la shule, Mwalimu Lenatus Njooka amesema kuwa wamekuwa wakikwama pale wanapotakiwa kufika mjini kwa ajili ya mahitaji ya shule.

Amesema kuwa shule yake awali ilikuwa na walimu watatu na kuwa baada ya kuongezwa kwa walimu katika shule hiyo walijitahidi kufundisha wanafunzi na hatimaye shule yake ya Iduchu kushika nafasi ya juu na kupata zawadi hiyo.

Aidha baadhi ya wakazi wa mkoani Njombe wamekuwa na mtazamo tofauti juu ya kuanzishwa kwa tuzo hiyo na kuwa hakuna uhusiano mzuri baina ya wazazi na walimu.