Alhamisi , 2nd Apr , 2015

Timu ya Yanga inatarajia kuondoka kesho Kuelekea nchini Zimbabwe kucheza mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho dhidi ya timu ya FC Platinum ya nchini Zimbabwe itakayochezwa April nne uwanja wa Mandava uliopo Gweru Bulawayo.

Yanga na Platinum katika mechi ya awali Taifa

Akizungumza jijini Dr es salaam , Kocha msaidizi wa timu hiyo, Boniface Mkwasa amesema, timu imejiandaa kwa ajili ya kupambana katika mechi hiyo ambapo wanaamini watafanya kama mechi ya awali iliyochezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Kwa upande wake, Nahodha wa Timu hiyo, nadir Haroub Canavaro amesema, mchezo huo utakuwa ni mgumu kwani mpira ni sayansi lakini uwezo wa kushinda ugenini ni mkubwa kuliko nyumbani.

Yanga waliifunga FC Platinum bao 5-1 katika mchezo wa awali ambapo hivi sasa wanatakiwa kupambana ili kusaka ushindi ugenini na kuweza kufuzu kwa hatua inayofuata ya timu 16.

Endapo Yanga itafanikiwa kuwatoa FC Platinum itaingia katika hatua ya 16 bora na itakutana na mshindi kati ya timu za Benifica de Luanda ya Angola au Etoile du Saleh ya Tunisia.