Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amepata Tuzo ya Presidential Global Water Changemakers 2025 ambayo alitunukiwa tarehe 13 Agosti, 2025 Cape Town, nchini Afrika Kusini.
Tuzo hiyo iliwasilishwa kwake na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Mahmoud Thabit Kombo, Ikulu Tunguu Zanzibar tarehe 26 Oktoba, 2025.
Tuzo hiyo ya Ulimwengu ya Marais wanaoleta Mabadiliko katika Sekta ya Maji imetolewa kwa kutambua uongozi bora na dhamira ya dhati katika kuanzisha na kuendeleza mipango na miradi ya Maendeleo katika Sekta ya maji nchini Tanzania.

