Jumatatu , 20th Oct , 2025

Jamhuri itajibu hoja nne za mapingamizi ya Lissu aliyotoa Ijumaa ya tarehe 17, Oktoba 2025 juu ya kukataa vielelezo vielelezo vilivyowasilishwa na shahidi namba tatu wa Jamhuri kuwa visipokelewe na mahakama.

Wakati kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu ikiendelea kuunguruma leo Jumatatu Oktoba 20, 2025 katika Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam, upande wa Jamhuri unatarajiwa kuanza kujibu hoja za pingamizi la Lissu kuhusiana na upokewaji wa video inayomuonesha akitamka maneno yanayodaiwa kuwa ya uhaini, ili iwe kielelezo cha ushahidi wa upande wa mashtaka.

Katika kesi hiyo Lissu anakabiliwa na shtaka la uhaini akidaiwa kutoa maneno ya kuitishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kinyume na kifungu cha 39(2) (d) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu.

Kesi hiyo inayosikilizwa na jopo la majaji watatu linaloongozwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Iringa, Dunstan Ndunguru, akishirikiana na majaji James Karayemaha na Ferdinand Kiwonde katika hatua ya ushahidi wa Jamhuri, itajibu hoja nne za mapingamizi ya Lissu aliyotoa Ijumaa ya tarehe 17, Oktoba 2025 juu ya kukataa vielelezo vielelezo vilivyowasilishwa na shahidi namba tatu wa Jamhuri kuwa visipokelewe na mahakama.