
Jaji Astrit Kalaja alifariki akiwa njiani kupelekwa hospitalini, maafisa walisema, huku wengine wawili waliohusika katika ya mzozo wa mali - baba na mwana - walipigwa risasi lakini walipata majeraha ambayo hayakuwa hatari kwa maisha.
Polisi wamesema walimkamata mshukiwa wa kiume mwenye umri wa miaka 30.
Waziri Mkuu wa Albania Edi Rama ametoa rambirambi zake kwa familia ya Jaji Kalaja Pia ametaka ulinzi mkali ndani ya mahakama za nchi hiyo na adhabu kali kwa watu wanaomiliki silaha kinyume cha sheria.
Mshukiwa wa mauaji ya Jaji Kalaja alifyatua risasi kwa sababu alitarajia kushindwa katika kesi hiyo, kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya eneo hilo.
Mjomba wa mtuhimiwa ni mlinzi wa mahakama, pia ameripotiwa kukamatwa kutokana na tukio hilo.
Mwendesha mashtaka mkuu wa Albania Olsian Çela alisema kufuatia tukio hilo kwamba usalama wa majaji unahitaji kuimarishwa "katika kila jambo".