Jumatatu , 30th Jun , 2025

Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA limechelewesha uamuzi wa mustakabaili wa Crystal Palace kushiriki michuno ya Europa League msimu ujao baada ya Jumamosi ya Juni 28 kutangaza kuwa maamuzi hayo yatafanyika leo Juni 30.

Palace walifanikiwa kufuzu kushiriki michuano hiyo baada ya kutwaa kombe la FA msimu wa 2024-2025 lakini nafasi yao ya kuiwakilisha England ipo hatarini kwa sababu ya sheria za UEFA za umiliki wa viabu vingi ambazo zinazuia timu zilizo chini ya umiliki mmoja kushiriki mashindano hayo ya Ulaya.

Mmiliki mwenza wa klabu hiyo John Textor ambaye pia anamiliki klabu ya Lyon ya nchini Ufaransa amekubali kuuza alimia 44 ya hisa zake katika klabu ya Crystal Palace ili kuirahisisha kesi hiyo inayowakabili.