Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye foleni ya kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa mfumo wa BVR.
Akizungumza na waandishi wa habari, Wilayani Makete, kaimu afisa uchaguzi wa wilaya ya Makete Gregory Emmanuel, alisema kuwa zoezi hilo linaenda vizuri katika halmashauri hiyo licha ya kuwepo changamoto mbalimbali za mashine.
Amesema kuwa kwa siku ya kwanza Machi 16 walifanikiwa kuwaandikisha watu 2153 katika vituo walivyo vitenga kulingana na mashine 38 walizo pewa na tume na zinazo fanya kazi ni mashine 36 huku mashine mbili zikibaki za ziada kwaajili ya dharura.
Emmanuel amesema kuwa halmashauri yake kuna vituo 36 ambavyo vimechukua kata 5 na siku ya pili walifanikiwa kuandikishwa 2479 na kuwa idadi ya watu imeongezeka kutokana na uzoefu unavyo ongezeka wa watu wanao andikisha.
Amesema kuwa katika halmashauri yake siku ya pili ameshuhudia mtu mmoja ambaye alishindwa kuandikishwa kutokana na usugu wa mikono yake na mashine kushindwa kuchukua alama za vidole vyake.
Amesema mtu huyo alitakiwa kurudi nyumbani kutokana na kushindwa kuchukuliwa alama zake za vidole na hajajua hatima ya mwananchi huyo kwa kuwa hajawasiliana na ye kama amerudi.
kituo hiki kimeshuhudia watu wakiwa wamehamashika na kuwa wavumilivu katika mistari ya kusubiri kuandikishwa na watu wakitumia dakika zaidi ya 15 hadi anapo toka na kitambulisho.
Baadhi ya wananchi wamesema kuwa wamekuwa wakiwahi katika vituo vya kujiandikisha wengi wao wakisema wanawahi foleni majira ya saa 11 alfajiri na kukuta wenzao wakiwepo katika foleni na kufikia majira ya saa Tano ndipo kujikuta wakiandikishwa.
John Sanga ni mmoja wa wakazi ambao waliwahi majira ya saa 11:00 alfajiri na kujikuta inafika saa 5:00 asubuhi kupata kitamulisho chake.
Baadhi yao wamekuwa na mtazamo tofauti juu ya vitambulisho hivyo huku wengi wao wakijiandikisha kwaajili ya kupigia kura pekee na wengine wakitaka kwaajili ya kutambulika.