
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya
Taarifa hiyo imetolewa leo Machi 5, 2025, na Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, na kusema kwamba kwa kipindi cha mwezi Februari jumla ya watuhumiwa 1,108 walikamatwa kwa tuhuma za makosa mbalimbali ikiwemo mauaji, kujeruhi, kupatikana na nyara za serikali, kupatikana na Pombe Moshi na kupatikana na dawa za kulevya.
Watuhumiwa walikamatwa wakiwa katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Bondeni iliyopo Mtaa na Kata ya Itewe wilaya ya Chunya wakiwa na noti bandia kumi na tano za shilingi elfu kumi kila moja ambazo kama zingekuwa halali ni sawa na shilingi 150,000/= zote zikiwa na namba CA 3903666.