
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Jacob Mwambegele
Tahadhari hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Jacob Mwambegele kwenye mkutano wa Tume na wadau wa uchaguzi kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura linalotarajiwa kufanyika kuanzia Machi 17 mpaka 23, 2025 kwa mkoa wa Dar es Salaam.
Amesema mtu mmoja anatakiwa ajiandikishe mara moja kwani mfumo wa uandikishaji wa mwaka 2025 umeboreshwa kwa kuzingatia alama za vidole, picha pamoja na sahihi hali ambayo mtu akijaribu kurudia inaweza kumtia hatiani.