Katika kozi hiyo, Kipa aliyewika katika timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars na klabu zote kubwa nchini Simba na Yanga SC atakuwa miongozi mwa watakaoshiriki kozi hiyo.
Kozi hiyo inatarajia kushirikisha makocha mbalimbali kutoka Tanzania Bara na visiwani lengo likiwa kupata makocha wa magoli kipa ambao watakuwa na uwezo zaidi wa kutoa mafunzo kwa magoli kipa kwa ajili ya kujiandaa kupambana katika mashindano mbalimbali yaliyo mbele yao.
Mbali na Kaseja, wengine ni Juma Nassor Pondamali, kocha wa makipa wa klabu bingwa Tanzania Bara, Yanga SC, Rafael Mpangala (Mgambo JKT), Adam Abdallah Moshi (Simba SC ), Khalid Adam Munnisson (Mwadui FC), Choke Abeid (Toto African), Mussa Mbaya (Ndanda FC), Idd Abubakar Mwinchumu (Azam FC), Herry Boimanda Mensady (Tanzania Prisons), Kalama Ben Lwanga (Stand United) na Patrick Mwangata (Mtibwa Sugar).
Wengine ni Abdi Said Mgude (Coastal Union), Razack Siwwa (African Sports Tanga), Josia Steven Kasasi (Mbeya City), Ramadhani Juma (Kagera Sugar Kagera), Abdallah Said Ngachimwa (JKT Ruvu), John Bosco (Majimaji FC Ruvuma), Fatuma Omary (Twiga Stars), Juma Kaseja Juma (Huru), Athuman Mfaume Samata (Ilala) na Peter Manyika John (Taifa Stars).
Hussein Tade Katadula (African Lyon), Juma Mohamed Bomba (Kinondoni), Mwameja Mohamed Mwameja (Ilala), Agustino Malindi Mwanga (Kigoma), Mohamed Abbas Silima (Police SC. Zanzibar), Bakari Ali Kilambo (Kizimbani SC Zanzibar), Hafidh Muhidin Mcha (Zanzibar Heroes), Elyutery Deodatusy Mholery (Kinondoni), Salim Waziri (Tanga)