Jumanne , 4th Mar , 2025

Dereva wa Mercedes  Andrea Kimi Antonelli amekataa  kwamba yeye ni mbadala wa  Lewis Hamilton katika timu hiyo ya F1 badala yake anataka kuweka historia mpya katika mwanzo wake wa udereva. 

Andrea Kimi Antonelli

Mtaliano huyo mwenye umri wa miaka 18 anaamini kuwa  Mercedes walimchagua Akucheza mashindano  yake ya kwanza msimu huu baada ya bingwa  mara saba  Lewis Hmilton kuhamia Ferrari .

"Ninashukuru sana kwa imani na nafasi niliyopewa na Mercedes nafahamu ni timu kubwa pia  bila shaka wana matarajio  makubwa na mimi  hivyo nitajaribu kufanya vizuri zaidi nisiwaangushe." Antonelli

Antonelli alijiunga na timu ya  vijana ya Mercedes akiwa na umri wa miaka 11 na akapandishwa hadi F1 baada ya msimu mmoja tu katika  F2.