Jumanne , 25th Feb , 2025

Aliyekuwa kocha wa Arsenal Arsene Wenger amesema anafurahishwa na mwenendo wa mshambuliaji wa Liverpool Mo Salah ambaye ameonekana kuwa bora siku hadi siku

Arsene Wenger - Kocha wa Zamani wa Arsenal

“Nilicheza  dhidi ya  Salah kipindi ambacho anatengeneza nafasi sita na anafunga goli moja, hivi sasa anatengeneza nafasi mbili na anafunga mabao mawili yaani ana uwiano mzuri katika ushambuliaji” Wenger

Salah mwenye umri wa miaka 32 msimu huu  amecheza mechi 27 za EPL na amefunga mabao 25 na kutoa pasi za mwisho 16 akihusika katika mabao 41 kati ya 64 waliyofunga Majogoo