Ijumaa , 21st Feb , 2025

Robin Van Persie amesaini  mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia Feyenoord inayoshiriki ligi kuu ya Uholanzi

Robin Van Persie - Kocha mpya wa Klabu ya Feyenoord

Van Persie ambaye aliwahi  kuwa mshambuliaji wa Arsenal na Manchester United anaenda kuiongoza klabu hiyo inayoshika nafasi ya 4 katika msimao wa Eredivisie akichukua nafasi ya Brian Priske aliyeondoka klabuni hapo wiki iliyopita

Feyenoord inakua timu ya pili kwa Mholanzi huyo mwenye umri wa miaka 41, tangu aanze rasmi kibarua cha ukocha 2024 akiwa na Heereveen inayoshika nafasi ya 9 katika msimamo wa ligi kuu nchini Uholanzi

Ikumbukwe Feyenoord ilikuwa klabu ya kwanza kwa  Robin Van Persie kuichezea katika soka la kulipwa mwaka 2001 kabla ya kutimkia Arsenal na alistaafu soka lake la kulipwa klabuni  hapo mwaka 2019.